Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Taasisi ya Bilal Muslim Tanga imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuyaenzi matukio ya kihistoria ya Kiislamu, jambo ambalo linaongeza chachu ya mwamko wa Tabligh ndani ya Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s).
Katika muktadha huu, Madrasatu Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) iliyopo chini ya Taasisi ya Bilal Muslim – Kanda ya Pangani, katika Kijiji cha Kasanga, leo tarehe 10 Mei 2025, imeandaa Hafla ya Kuzaliwa kwa Imam Ali Ridha (a.s.), hafla iliyopambwa pia na Maonesho ya Wanafunzi wa Madrasa kutoka maeneo mbalimbali.
Hafla hii imehudhuriwa na Madrasat kutoka Bilal Muslim – Kanda ya Pangani pamoja na baadhi ya Madrasa kutoka kwa ndugu zetu wa Kisuni. Hili ni jambo la faraja kubwa, linaloashiria mshikamano wa kijamii na wa kidini katika maeneo yetu.
Kwa heshima na taadhima, Kitengo cha Ripoti za Tabligh kutoka chini ya Hauzat Imam Ali (a.s) Pangani, kinatoa shukrani za dhati kwa uongozi wa Taasisi ya Bilal Muslim Tanga kwa kuendelea kupanua wigo wa elimu ya dini na Tabligh kwa njia ya vitendo.
Habari hii ni kwa hisani kubwa ya:
Kitengo cha Ripoti za Tabligh – Bilal Muslim Pangani.
Kwa niaba ya: Madrasat Imam Jafar as-Sadiq (a.s), Kasanga.
Your Comment